Posts

Showing posts from 2017

Video: Combination ya Matic na Pogba

Image
Wachezaji Matic na Pogba wameonyesha ushirikiano mzuri msimu huu katika sehemu ya kiungo na kuing'arisha timu yao licha ya kutoka sare katika mchezo wao wa mwisho dhidi ya Stoke huku United wakishindwa kuivunja record ya kutoweza kuwafunga Stoke katika uwanja wao wa nyumbani tangu mwaka 2013 yani alipostaf kocha Ferguson katika klabu hiyo. Wachezaji hao wameonyesha kuelewana mapema kama vile walicheza pamoja kwa miaka mitano iliyopita kiasi cha kuwafanya wapinzani wao kuwa na wakati mgumu kwa muda wote kama inavyoonyesha video hii hapa

Jinsi Lukaku alivyoibadilisha Man united mapema tu msimu huu

Image
Kinachoonekana Man United msimu huu ni tofauti na msimu uliopita licha ya mabadiliko madogo tu alioyafanya Mourinho kwa kuwasajili wachezaji ambao hata hivyo mmoja kati yao ameshindwa kupata nafasi kikosini hadi sasa licha ya kuwa wamecheza michezo mitatu ambaye ni Lindelof.  Jina la Lukaku si geni machoni na masikioni mwa watu hususani wapenzi wa ligi kuu ya Uingereza alichokikosa mchezaji ni ladha na utamu wa Champions League (kombe la vilabu vya ulaya) lakini hata hivyo alichokifanya Uingereza huwezi kuwa na mashaka nae juu ya mashindano haya makubwa barani Ulaya na duniani kote mchezo huyo amefanikiwa kufunga magoli matatu katika mechi tatu za mwanzo za ligi na ni manne tukijumuisha mashindano yote yani likiwemo na lile alofunga dhidi ya Madrid.    Lukaku ameifanya Manchester United iwe tishio zaidi mbele tofauti na ilivyokuwa msimu uliopita ikiongozwa na Ibrahimovic wachezaji hawa wote ni wafungaji wazuri lakini Lukaku ni mzuri zaidi licha ya kufanikiwa kufunga mag...

Man united yafanya hatari katika tuzo za ligi kuu Uingereza

Image
Lukaku ametajwa katika majina wachezaji watatu waliochaguliwa kugombea mchezaji bora wa mwezi wa nane(August) huku Manchester ikifanikiwa kutoa majina manne likiwemo la kocha Jose Mourinho anaegombea tuzo ya kocha bora wa mwezi huku mengine yaliotajwa ni Phil jones na Mkhitaryan. Lukaku aliekuwa mchezaji wa Everton amefanikiwa kufunga magoli matatu hadi sasa katika mechi tatu alizocheza ukiacha majina hao wengine wanaogombea ni Morata wa Chelsea, Saido Mane na Salah wote wakiwa wachezaji wa Liverpool na kipa wa Huddersfield aitwae Jonas Lossl.

Mourinho amsifu Pareira kwa kuongeza mkataba mpya

Image
Pareira ameongeza mkataba wake wa kukipiga OT licha ya kusajiliwa na Valencia ya Spain kwa mkopo mwishoni mwa dirisha kubwa la usajili. Mkataba huo mwaka ambao utamuweka klabuni hapo hadi msimu wa mwaka 2018- 19.             Mou amemuelezea kijana huyo kama atakuwa mchezaji mkubwa na tegemeo hapo baadae mreno huyo amesema.   "Pareira ni mchezaji mzuri tayari ni mchezaji mdogo mwenye uwezo wa hali ya juu na mwenendo mzuri katika kuendeleza kipaji chake"   "Sina mashaka kuwa atakuwa mmoja ya wachezaji wakubwa wa hii klabu"     Pareira baada ya kujiunga na Valencia alisema   "kocha anatengeneza timu nzuri hapa na mimi nataka niwe sehemu ya hiyo timu hivi karibuni"    "Nitaendeleza uwezo wangu hapa Valencia na natumaini nitapata muda mwingi wa kucheza"  Pareira amecheza mechi 13 katika timu wa kubwa na kufanikiwa kufunga goli moja mechi yake ya kwanza ilikuwa dhidi ya Tottenham march 2015.

Wenger nusu awe kocha Manchester united

Image
Arsene Wenger alipata nafasi ya kuifundisha Manchester United baada ya Fergie kubwaga manyanga lakini hata hivyo aliikataa kutokana na utiifu wake kwa mwenyekiti wa Arsenal, David Dein amefichua Mwenyekiti wa zamani wa Manchester United Martin Edwards kuwa Wenger alikuwa ni chaguo letu la kwanza baada ya Ferguson kutangaza kustaafu msimu wa  mwaka 2000/01 kabla ya Fergie kubadili maamuzi na kuendelea kufundisha kwa zaidi ya miaka 10 yenye mafanikio makubwa. Martin asema kuwa "Tulimfata Wenger na alionyesha kuvutiwa na ofa yetu kiasi cha kutukutanisha mimi na Peter Kenyon katika nyumba yake London ili kusikiliza ni vipi tungezungumza." Edwards anaendelea kuwa kilichomfanya Wenger abaki ni utii wake kwa uongozi wa Arsenal kwa sababu Wenger alikuwa karibu sana na David Dein kitu kilichomfanya ashindwe kuondoka bila ya ridhaa ya uongozi wake.

Lindelof kuanzishwa mechi hii

Victor Lindelof ni moja ya majina mapya ambayo Mourinho ameyasajili msimu huu lakini mchezaji huyo ameshindwa kupata nafasi ya kucheza tangu ligi ianze huku Manchester wakiwa tayari wameshacheza michezo mitatu ndani ya ligi kuu ya mchezo, hata hivyo Lindelof sio mchezaji pekee aliyekosa nafasi ya kucheza kwani kuna kubwa jingine kama vile beki mwingine wa kati anayetambulika kwa jina la Smalling wote wawili wanatarajia kuanza katika mchezo wa klabu bingwa dhidi ya Basel kwa mujibu wa kocha wa klabu hiyo Jose Mourinho ameweka wazi kuwa atawaanzisha wachezaji wote wawili katika mechi hiyo ya klabu bingwa. Mourinho amesema atakuwa amesema kuwa Lindelof in mchezaji mzuri lakini hana uzoefu na ligi kuu ya Uingereza hivyo anahitaji muda wa kuzoea na kuingia katika mechi zijazo. Lindelof si mchezaji wa kwanza kufanyiwa kama hivyo na Mourinho wapo wengine waliosubirishwa ili waongeze viwango vyao kama vile Wilian akiwa na Chelsea Mikhtaryan na Martial akiwa Manchester.

Man united kumuiba Alexis Sanchez

Image
Manchester united wanafanya mawasiliano ya chini kwa chini na wakala wa Sanchez ili kufanikisha usajili wa kushtukiza kwa kuwapora wapinzani wao wakubwa katika jiji la Manchester klabu ya Manchester City ambao tayari wameshafanya mazungumzo nae. Alexis amekuwa njia panda katika dirisha hili la usajili baada ya kugoma kuongeza mkataba mpya katika klabu yake ya sasa ya Arsenal ili atue klabu mpya yenye kiu ya mataji na itayoshiriki klabu bingwa. Mourinho ni mshabiki mkubwa wa mchezaji huyo raia wa Chile lakini ni kazi ngumu kumsajili mchezaji kutokana na uwepo wa kocha Guardiola katika klabu ya Manchester city aliewahi kufanya kazi na mchezaji huyo katika klabu ya Barca. Sanchez ataelekea Man united kama mbadala wa Perisic baada ya kushindwa kumsajili kutoka Milan ya Italy inayokaribia kumuongezea mkataba hivi karibuni.

Evra atoa povu lake mtandaoni

Image
Mchezaji wa zamani Manchester ambae haishiwi na vituko mitandaoni Patrice Evra ameibuka tena mpya baada ya kuwaponda wanaomzarau akiwemo na mwalimu wake mwalimu wake aliemwambia kuwa huwezi soka kwa sababu wewe ni mfupi. Evra amezoweleka kwa kutumia video mbalimbali mtandaoni akisema maneno kama "I love this game" akimaanisha kuwa huu mchezo naupenda mara hii amekuwa tofauti baada ya kutuma video inayomuonyesha akiwa mazoezini huku akisema "usiwe na wivu japo walisema siwezi sasa nina vikombe zaidi ya 21 nimecheza fainali nyingi na nimeshinda japo nimepoteza nyingi lakini nimeshinda makombe mengi na bado nahitaji makombe mengi zaidi" na akimaliza kuwa "I love this game"

Taarifa mpya za klabu ya Manchester United

Image
                   Antoine Griezman Wakala wa zamani wa Griezman amefichua kuwa ilibakia kidogo kwa mchezaji kujiunga na klabu ya Man united baada ya klabu yake anayoichezea ya Atletico Madrid kufungiwa kutokusajili. Taarifa zikisema kuwa klabu zote mbili zilikubaliana usajili wa mchezaji huyo kwa dau la euro milioni 100. Ivan Perisic Mchezaji anaewindwa vikali na klabu ya Manchester United Perisic, 28, anategemea kuongeza mkataba na klabu yake ya Inter Milan baada ya timu hiyo ya jiji la Milan kugoma kuwauzia mabingwa wa kombe la FA na Europa Man United. Milan watamuongezea mkataba hivi karibuni ili kuwakatisha tamaa Mashetani juu ya kumsajili winga huyo machachari.                     Luke Shaw Beki wa kushoto raia wa Uingereza Luke Shaw anatarajia kuongezewa mkataba wa kuendele...

Leicester yataka kumsajili Smalling

Image
Leicester city inataka kumsajili beki wa Manchester, Chriss Smalling kocha wa Leicester tayari ameshamsajili beki wa Hull city, Harry Maguire, 24, alieitwa na timu ya taifa ya Uingereza hivi karibuni na sasa anataka kumchukua raia mwingine wa Uingereza, Smalling aliekosa nafasi ya kucheza mara kwa mara tangu atue kocha Jose Mourinho na kumsajili Baily anayecheza sambamba na Jones wameonyesha ushirikiano mkubwa kiasi cha kuifanya Man United ishindwe kufungwa goli hata moja katika michezo yake mitatu ya mwanzo huku ikijikusanyia magoli kumi katika mechi hizo na kukiwa bado na ingizo jipya anaecheza pia nafasi ya beki wa kati kama Smalling aitwae Lindelof raia wa Sweden hivyo kuzidi kuwa na nafasi finyu katika timu hiyo ya Mashetani wekundu. Kocha wa Foxes, Shakespeare anataka kuiongezea makali safu yake ya ulinzi kwa kumsajili beki huyo raia wa Uingereza anayeonekana kukosa nafasi katika timu hiyo ya Man united kwa sasa ili kuirejesha katika ushindani kwenye ligi kuu ya Uingereza. Je ...

Nataka kusajili mchezaji wa nne maneno ya Mourinho

Image
Kocha Jose Mourinho ameweka bayana kuwa anataka kusajili ingizo jipya kwa kumsajili mchezaji wa nne lakini hata hivyo amesema kuwa hana haraka na hilo na hatawashinikiza bodi kufanya hivyo licha ya kuwa tayari ameshawasali wachezaji watatu ambao ni Lukaku, Matic kutoka kwa mahasimu wao Chelsea na Lindelof kutoka Benfica. Alisema "Inawezekana hata dirisha lijalo la usajili nikampata mchezaji wa nafasi ninayoihitaji ili kukiongezea makali kikosi changu" Manchester united wanaongoza ligi wakiwa na point 9 na magoli 10 huku wakiwa hawajafungwa hata goli moja katika michezo yao mitatu ya mwanzo msimu huu.

Mou amuonya Anthony Martial

Image
Mourinho hakusita kummimiminia sifa mshambuliaji wake Anthony Martial baada ya kuonyesha kiwango kizuri msimu huu na kufanikiwa kufunga mabao mawili na assist moja katika michezo yake mitatu ya mwanzo ya ligi kuu ambapo miwili kati yao amekuwa akiingia ndani ya uwanja kama mchezaji wa akiba. Mourinho alisema "Nadhani kuwa unapokuwa na kipaji huwezi kukiacha kipotee unapojaaliwa kipaji inabidi ukitumie kipaji chako na kukiendeleza bila ya kukiacha kipotee kipaji hicho." "Nahitaji kuona zaidi kutoka kwake kwa sababu ana vitu vyote hivyo nafikiri ananielewa zaidi kwa sababu tuna uhusiano mzuri tu"

Mkhtaryan na record mpya dhidi ya Leicester

Image
Mkhtaryan aweka record baada ya mchezo wake dhidi ya Leicester kwa kutoa assist kwa mchezaji Rashford na kuwa mchezaji pekee kufanya hivyo kwa kutoa assist tano katika michezo mitatu ya mwanzo ambapo imekuwa ni haraka zaidi kwa mchezaji wa ligi kuu ya Uingereza kuwahi kufanya hivyo akiwa sambasamba na Ruel Fox wa Newcastle aliyefikisha pasi kama hizo za magoli tano katika michezo mitatu ya mwanzo tokea msimu wa 1994/95. Mkhtaryan alitoa pasi mbili katika mchezo wao wa kwanza dhidi ya West ham kwa kutoa assist kwa wachezaji Lukaku na Martial na kuendeleza kazi yake hiyo katika mchezo uliofuata dhidi ya Swansea akitoa tena pasi mbili kwa wachezaji Lukaku na Pogba na akimaliza kazi yake kwa Leicester mara hii akitoa assist kwa Rashford huku Klabu ya Manchester ikifikisha magoli 10 katika michezo mitatu.

Tetesi za usajili Man united

Image
Tottenham na Inter Milan kwa pamoja zimeingia katika mbio ya kumuwania beki wa PSG na anaewindwa na Manchester united Sergi Aurier beki huyo wa PSG na Raia wa Ivory coast anahusishwa vikali na kujiunga na Man utd. Chanzo : La Parisien Klabu ya Manchester united inamfatilia kiungo wa Anderlecht aitwae Leander Dendocker. Mashetani hao wekundu wametuma scout ili kumfatilia kiungo ambae alifunga goli walipokutana na timu hiyo katika mashindano ya Europa League, mchezaji huyo kwa sasa ana miaka 22, Kocha wa united anamtaka kiungo huyo kwa msimu ujao. Lakini pia mchezaji huyo anawindwa na klabu za Leipzig na Ac Milan ya Italia. Chanzo : The Mirror                 Klabu ya Watford inataka kumsajili kinda wa Man utd Timothy Fosu-Mensah kwa mkopo kinda wa United mwenye uwezo wa kucheza kama beki wa pembeni,kiungo mkabaji na beki wa kati hatma yake kuamuliwa baada ya mchezo wa dhidi ya Real Madrid. Chanzo : Dail Mail       ...

Officially Matic kwenda Man united asema haya baada ya kusaini

Aliekuwa kiungo wa Chelsea amekamilisha usajili wa kuelekea United kwa dau la £40m na kuwa mchezaji wa tatu kusajiliwa na klabu huku akionyesha kuwa na furaha kufanya tena kazi na mreno huyo Matic alinena kufanya tena kazi na Mourinho ilikuwa ni bahati ambayo nisingeweza kuikataa ninachosubiri ni  kuanza kazi hapa kufanya mazoezi na kucheza mechi hapa pia hakuacha kushukuru klabu na  mashabiki wa timu ya Chelsea kwa ushirikiano wao. Kocha Jose Mourinho alimkaribisha mchezaji huyo klabuni hapo klabu hiyo imesajili wachezaji watatu kwa £150m.

Man united yaichabanga Valerenga 3 - 0 pamoja na video ya magoli yote

klabu ya Manchester united jana iliendeleza ubabe wake ya kutoka kupoteza kwa Barcelona katika mechi za kirafiki zilizopigwa Marekani ambapo mpaka sasa Manchester wamepoteza mchezo moja tu katika michezo yote sita waliocheza ya kujiandaa kwa msimu ujao huku maingizo mapya kama Lukaku na Lindelof wakiendelea kung'ara vyema. Katika mchezo wa jana jumapili United walifanikiwa kuichabana valerenga kwa magoli matatu yaliofungwa na wachezaji Fellaini, Lukaku na Mctominay aliemalizia pasi nzuri kutoka kwa Martial kufanya matokeo kuwa tatu bila.      

"Ni rahisi kunisajili mimi lakini sio Fellaini" Mourinho

Image
Mourinho akana taarifa zinazoenea kuwa Maroune Fellaini atajiunga na galatasaray kwa kusema kuwa Galatasaray ni rahisi kunipata mimi na kama wanahitaji kocha nafasi ipo lakini sio Fellaini ni mchezaji muhimu sana kwangu baada ya mchezaji huyo kufunga goli katika ushindi wao wa magoli 3 - 0. Licha ya hivo mchezaji huyo amebakiza mwaka mmoja tu katika mkataba wake na klabu hiyo huku Matic akikaribia kusaini katika klabu hiyo akitokea chelsea kwa mujibu wa taarifa.

Matic kumalizana na Manchester united

Image
Imethibitishwa na sky kuwa matic anakaribia kujiunga na Manchester na muda wowote kuanzia sasa atafanyiwa vipimo vya afya Matic anatarajia kufanya kazi tena na kocha Jose Mourinho baada ya kutengana nae mwaka 2014 wakati ambao Mourinho alitolewa muhanga na Abrohmovic baada ya mwenendo mmbovu wa klabu hiyo na mwaka 2016  Mou akajiunga na mahasimu wakubwa wa klabu ya Chelsea  jiji ya la London ambayo  ni klabu ya Manchester united. Matic ni chaguo la kwanza kwa kocha Jose Mourinho katika nafasi ya kiungo mbele ya mchezaji Fabinho, kocha huyo mreno amesema wazi kuwa anahitaji kiungo wa kati na mshambuliaji mmoja wa pembeni ili kuanzisha nafasi ambayo anahushwa Perisic wa Inter Milan.

Renato Sanchez anukia Manchester United

Image
Baada ya kocha wa Bayern Munich kusema kuwa mchezaji wa timu hiyo Renato Sanchez anaweza kutimkia timu nyingine katika dirisha hili kubwa la usajili mara hii ni mchezaji mwenyewe Sanchez ambae amethibisha kuwa anaondoka msimu huu na kutimkia timu nyingine ili kupata nafasi ya kucheza mara kwa mara, Sanchez amesema maneno hayo baada ya kumalizika kwa mchezo wao dhidi ya Chelsea na kuichabanga kwa magoli 3 kwa 2. Bayern hawapo tayari kumuuza mchezaji badala yake wanategemea kumpeleka kwa mkopo kwa mashetani wa jiji la Manchester huo utakuwa ni usajili wa tatu kufanywa na klabu hiyo ambayo pia inawawania wachezaji kama Marco Verrati na Perisic. Sanchez aliwahi kuikacha Manchester united na kabla ya kusaini Bayern lakini kikwazo ni kuwa pia kinda huyo anawindwa pia na klabu ya AC Milan ya Italia ambapo akiizungumzia Milan amesema yupo tayari kujiunga nao endapo watatoa ofa sahihi kwa klabu yake na kukubaliana pande zote mbili kwa kusema AC Milan atapata nafasi zaidi ya kucheza kuliko Bay...

Carrick amtaja atakaerithi ukapteni baada ya yeye kustaafu

Mchezaji wa Manchester united ambae ni kapteni kwa sasa Michael Carrick amemtaja mrithi wake baada ya yeye kustaafu kwa kumtaja Pogba kama mbadala wake baada ya yeye kustaafu lakini jambo hilo linaweza kumuongezea presha mchezaji huyo aliesajiliwa kwa dau nono kwa kurejea tena mara hii akitokea Juventus. Klabu ya Manchester ilipata skendo ya kuwa ilitumia njia za panya kumsaini akitokea Le Havre na kusemekana kuwa ingehukumiwa kwa kufungiwa kusajili lakini hata hivyo dai hilo lilitupiliwa mbali kwa kukosa ushahidi na mwaka 2016 akirejea tena kwa dau nono lililozuwa maneno na vijembe kutoka kwa waandishi na wachambuzi wa soka kabla ya kufanikiwa kutwaa vikombe vitatu ambavyo ni ngao ya jamii, kombe la ligi na Europa ndogo. Kocha Jose Mourinho amekataa kutaja kapteni msaidizi mwaka huu tangu Rooney atimkie katika klabu yake ya utotoni ya Everton na Carrick kurithi beji hiyo huku akiwa na umri wa miaka 36. Swali ni je Pogba ni mtu sahihi wa kurithi beji hiyo?

Man united kusajili watatu wiki hii

Image
Mtendaji mkuu wa klabu ya Manchester united Ed  Woodward amebaki jijini ili kuhakisha kuwa anakamilisha biashara ya kuwasajili wachezaji watatu ndani ya wiki hii taarifa kutoka mtandao wa Manchester Evening News imesewa kuwa Woodward alitakiwa kuhudhuria mjini Houston ili kushuhudhia mchezo wa Manchester derby lakini ameshindwa kutokana na majukumu yake ya kazi ili kuhakikisha kuwa anafanikisha dili la wachezaji Dier,Perisic na Matic  au wawili kati yao na ikishindikana wawili basi hata mmoja wao mapema wiki hii. Kocha huyo mbwatukaji wa Manchester united kwa sasa bado hajaonana na mtendaji huyo tangu aseme waziwazi kuwa hafurahishwi na utendaji wa kazi wa klabu yake katika idara ya hiyo kwa kushindwa kuwasajili mapema orodha ya majina ya wachezaji alioiwasilisha.

Viwango vya wachezaji wa Man United na video highlight ya mchezo dhidi ya Man city

Image
Kocha Jose Mourinho amepambana tena na Guardiola na kuibuka na ushindi wa goli mbili kwa bila na mchezaji Lukaku akiendelea kung'ara tena na kufunga goli moja katika mchezo huo. Hivi ni viwango vya wachezaji wa man united katika mchezo wa leo. De Gea : Ameokoa michomo miwili hatari kuifanya Man united iendelee kuongoza. 4/5 A.Valencia : Alipanda na kushuka golini kwa kasi kuisaidia timu vizuri mchezaji alieanza kama kapteni wa timu kabla ya kumpa Carrick kipindi cha pili. 4/5 V.Lindelof : Alifanya kosa moja kiasi liigharimu timu, Alikuwa ni mwiba mkali kwa Aguero kwa kumkaba vilivyo. 3.5/5 D.Blind : Hakuwa fomu siku ya leo, na kuhenyeshwa vilivyo na Patrick Roberts kwa mtazamo ni vyema akicheza kati. 3/5 C.Smalling : Kuna wakati alicheza vizuri lakini kuna wakati aliharibu na ilikuwa ni bahati kwake kutowapa city penati. 3/5 P.Pogba : Ana uwezo mkubwa wa kutoa pasi aliwasumbua sana wachezaji wa Manchester city na vitu vyake vingi na adimu kuviona kwa mchezaji. 4/5 H....

Usajili wa Perisic kuelekea Man utd hauzuiliki

chezaji Perisic ameamuwa kutumia njia ya kugomea klabu yake kwa kutosafiri kwenda china kwa ajili ya mechi za maandalizi ili kuifanya ikubali kumuuza kwa Manchester United. Kwa taarifa za ndani ya klabu ya Inter Milan ni kuwa klabu hiyo imeanza mchakato wa kumsaini mchezaji Keita Balde kutoka Lazio ya Italia ili kwenda kuziba pengo la Perisic atakapojiunga na Mashetani wa jiji la Manchester. Perisic amepewa ruhusa ya kutohudhuria mazoezi ya klabu hiyo na kwenda nchini kwao croatia kumuona dokta meno. Perisic atakuwa ni wa tatu kusajiliwa kati ya wachezaji wanne ambao Mourinho anataka kuwasajili msimu huu.

Takwimu ya wachezaji wa Man United dhidi ya Real Salt

Image
J.Pereira : Ameokoa michomo miwili hatari japo alifungwa lakini ni goli ambalo hata kipa bora duniani angeweza kufungwa. 3.5/5 P.Jones : Alikosa umakini kidogo kiasi cha kuigharimu timu hadi kufungwa. 2.5/5 D.Blind : Hana kasi kubwa katika kupanda na kushambulia huku akirudi nyuma kulinda goli lakini ni mchezaji ambae ana uwezo mkubwa wa kukaba kama alivyofanya leo.2.5/5 V.Lindelof : Amerudi tena leo kwa mara ya pili na kama ilivyo kawaida yake alitulia uwanjani na kutoa pasi nzuri kama linavyosema jina lake la utani mtu wa barafu(iceman). 3.5/5 T.Fosu-Mensah : Alionesha ubora wake kwa kulinda huku akipanda na kushuka alikuwa pia akishirikiana vizuri na wenzake wenzake uwanjani. 3.5/5 S.Mctominay : Ameonyesha kujiamini uwanjani na hakusita kwenda mbele kila alipopata mipira. 3.5/5 M.Carrick : Hakuwa katika ubora wake leo kwa kushindwa kumiliki mipira. 2/5 P.Pogba : Alipoteza mipira mingi uwanjani lakini baadae alibadilika na kucheza vizuri kiasi. 2.5/5 H.Mkhtaryan : Ame...

Video ya Andreas Perreira dhidi ya LA Galaxy

Image
Mchezaji Andreas ameonyesha kukomaa tayari baada ya kuonyesha makali uwanjani kwa utulivu wa hali ya juu pindi anapokuwa na mpira na pasi za uhakika na zenye macho ya kumuona mlengwa haya ni baadhi ya matukio yake uwanjani katika mchezo wa leo dhidi ya wapinzani wao LA Galaxy ambao waliwahi kuwafunga goli saba katika mchezo uliopita na kufanikiwa kuwafunga tano katika mchezo wa leo.

Takwimu ya wachezaji wa Man utd baada ya mchezo dhidi ya LA Galaxy

Image
Manchester United imeanza vzuri mechi yake ya maandalizi baada ya kuichabanga klabu ya LA Galaxy ya Marekani kwa mabao 5 kwa 2 katika mchezo huo ambao Mourinho alichezesha vikosi viwili tofauti ili kuipima timu yake vizuri. Huu ulikuwa ndio mchezo wa kwanza kwa wachezaji Lukaku na Lindelof kwenye timu yao hiyo mpya na hizi ndio takwimu za mchezo huo. De Gea : Hakuokoa mchomo wowote katika mchezo huo lakini bado umuhimu wake ulionekana katika kuanzisha mashambilizi kwa kutoa pasi nzuri. 2/5 Daley Blind : Hakupata matatizo sana kiulinzi lakini msaada ulikuwa pale alipotoa pasi nzuri za mbele katika kusukuma mashambulizi mbele ya timu pinzani. 3/5 Chris Smalling : Smalling hakuwa pembeni alicheza kama beki wa kati aliziba njia za wapinzani kupita alionyesha kujiamini na kucheza kwa uangalifu mkubwa. 3/5 Phil Jones : Hakuwa na mambo mengi uwanjani lakini aliwajibika vizuri katika kuzuwia hatari zote golini. 3/5 Anthony Valencia : Aliwazima wapinzani katika upande wake wa kulia na...

Martial video yake mazoezini (A.Martial amazing assist at training video)

Image
Anthony Martial aonyesha ubora wake mazoezini jana kwa kutoa assist ya kisigino hatari kwa mchezaji mwenzake Marcus Rashford na kutupia nyavuni klabu ya Manchester United ipo nchini Marekani kujiandaa na mechi za kirafiki huku wachezaji wakijitahidi kuonyesha wao ili kumvutia kocha Jose Mourinho wakiwemo Martial alieshindwa kumvutia kocha huyo msimu uliopita

Mama wa Ferdinand afariki dunia

Mama wa Rio na Anthony Ferdinand afariki dunia baada ya kusumbuliwa na Cancer. Bi Janice st Fort aliekuwa na miaka 58 alifariki dunia hospitalini akiwa na familia yake pembeni habari hizi zimekuja miaka miwili tu baada ya aliekuwa mke wake Ferdinand kufariki dunia na Cancer ya ziwa.  Wanafamilia wakitoa maneno yao ya mwisho baada ya mazishi karatasi ilisomeka hivi. "Tuna huzuni kuwaarifu kuwa mama yetu kipenzi Janice amefariki leo baada ya kusumbuliwa na Cancer. Alikuwa ni mtu muhimu kwetu na aliependwa na kila aliemjua. Alifariki dunia katika hospitali ya Guy's Cancer Unit, iliyopo London bridge. Alopoteza maisha huku akiwa na mume wake mpendwa Peter pamoja na sisi watoto wake wanne kando ya kitanda chake. Na wakimalizia kwa kutoa pongezi kwa wafanyakazi wote wa hospital hiyo ya Guy's Cancer Unit kwa kumhudumikia mama huyo kwa kipindi chote alichougua hapo. Ferdinand alimpoteza mke wake Rebeca Ellison mwaka 2015 huku mama yake bi Janice akifariki miaka miwili baad...

Inter Milan wavunja ukimya juu ya Perisic

Klabu ya Inter Milan yavunja ukimya na kuzungumzia habari za usajili zinasombaa kumhusu Perisic. Klabu ya Manchester United inahaha kusaka saini ya kiungo mshambuliaji hasa baada ya kuondoka kwa Wayne Rooney na huku mchezaji huyo wa Inter Milan akipewa nafasi kubwa kujiunga na mashetani hao wekundu wa jiji la Manchester. Kupitia chombo cha habari cha sky sport ya Italy kimetoa taarifa mpya juu ya ishu hiyo wakati akizungumza na vyombo vya habari Piero Ausilio mwenye cheo cha sporting director katika klabu hiyo ya Milan alisisitiza kuwa hakuna dili yoyote kati yao na Man united.   "Haiwezi kutokea" kama alivyonukuliwa na sky Italy "Perisic anafanya mazoezi na sisi hivyo hatuwezi kukubali ofa yoyote watakayoiwasilisha kwetu" Perisic mwenye umri wa miaka 28 raia wa Croatia kama akifanikiwa kujiunga na Manchester United atakuwa ni mchezaji wa tatu kujiunga baada baada ya Lindelof kutoka Benfica na Lukaku kutoka Everton.    Tupia comment yako chini apo bila ya mash...

Sky Sport : Perisic kusaini Man United hivi karibuni

Mchezaji wa Inter Milan Perisic anataka kujiunga na Manchester United na wakala wake amekutana na Inter Milan siku ya jumatano kwa mazungumzo chanzo; Sky sport  Sky Sport imeripoti kuwa Manchester United wanakaribia kumsaini mchezaji huyo huku Inter Milan wakigomea katika dau la Euro milion 48 na klabu ya Manchester ikishindwa kufikia dau hilo huku kikiendelea kuripoti chombo hicho ni kuwa klabu ya Manchester imekwamia katika dau la Euro millioni 39 na kutarajia kuongeza hadi kufikia Euro milioni 45 kwa kiungo aliebakiza miaka mitatu katika mkataba na klabu ya Inter Milan aliyojiunga nayo mwaka 2015 akitokea Wolfsburg ya Ujerumani na kufanikiwa kuifungia klabu yake hiyo ya Inter Milan magoli 18 katika michezo 70 na kocha wa Inter Milan akisema kuwa anataka kumsikia mchezaji huyo mwenyewe akisema kama anataka kuondoka hapo ndio atoe maamuzi yake yeye kama kocha lakini matumaini yake makubwa ni kuwa atabaki nae kwa msimu ujao na huku mabingwa wa kihistoria wa ligi kuu ya Uingereza w...

Rooney aaga rasmi na wachezaji wakitoa maneno yao

Image
Safari ya aliekuwa mchezaji wa Manchester united Wayne Rooney imefika na amekamilisha usajili wake na kurudi katika klabu yake ya utotoni ya Everton. Rooney ameiaga rasmi klabu yake hiyo aliochezea muda mrefu  Manchester ambayo ilimsajili kutoka Everton mwaka 2004 na akaitumikia kwa muda wa miaka 13 huku akishinda vikombe 16 na kuvunja record ya ufungaji katika klabu hiyo. Ametuma katika mitandao kijamii amesema "Nataka kutoa shukran kubwa kwa kila mtu hapa Manchester" "Shukran kwa bodi nzima, na makocha niliocheza chini yao, na wafanyakazi wote tuliofanya kazi pamoja, na wachezaji wote tuliocheza pamoja na mwisho ni mashabiki wazuri ambao nimebahatika kucheza chini yao, Ahsanteni." Baada ya hapo ni wachezaji ambao amecheza nao walionyesha hisia zao kupitia mitandao ya kijamii kama vile Daley Blind: Kila la heri @WayneRooney and na asante kwa kila kitu. #Gwiji Tim Fosu-Mensah: Kwaheri gwiji, @WayneRooney. Nahisi kuheshika kwa kuweza kucheza na wew. #Legend An...

Ivan Perisic athibitisha kusajiliwa na Man united

Image
Baada ya kukamilisha usajili wa Lukaku sasa klabu ya Man united inatazamia kukamilisha usajili wa winga machachari Ivan Perisic baada ya mchezaji huyo wa Inter Milan kuthibitisha hilo kwa vitendo katika mtandao wa kijamii ambapo tangu juzi taarifa kubwa iliotawala ni juu ya aliekuwa mshambuliaji wa Everton Lukaku kusajiliwa na man united kwa dau la paund milion 71. Perisic kwa kuonyesha mapenzi yake na klabu ameanza kwa kumfollow Lukaku katika account yake ya Instagram akiendelea kwa kuzi like picha ambazo Lukaku na Pogba wamepiga wakiwa pamoja                                                       Huku bila ya kuishia hapo aliweka nukta nyekundu katika profile account yake ya Instagram rangi inayotumiwa na Manchester united huku tukirudi nyuma kabla Perisic hajasiliwa na Inter Milan mwaka 2015 ni account hiyo hiyo aliweka nukta m...

Pogba ampongeza Lukaku

Image
Kiungo wa Manchester united, Paul Pogba amemkaribisha Romelu Lukaku katika account yake ya Instagram. Paul Pogba ametuma video yake akimpongeza mshambuliaji huyo kwa kukamilisha wake uhamisho wake na kuungana na rafiki yake huyo wa muda mrefu.                https://www.instagram.com/p/BWRuiuthRnJ/?r=wa1 Katika video ambayo Pogba ameandika "tutaonana kesho mazoezini" baada ya klabu ya Manchester united kuthibisha kumsajili aliekuwa mshambuliaji wa Everton Lukaku. Lukaku akiongea kifaransa anasema "haikuwa kazi rahisi, lakini sasa tumekamilisha, tutaonana kesho. Pogba anamuuliza "umesemaje" Lukaku anamjibu "tutaonana kesho, Unaamini au? Pogba kwa sauti anajibu "ndio mzee". Lukaku na Pogba wote kwa pamoja wapo Los Angeles ambako lukaku anarajia kufanyiwa vipimo vya afya na kujiunga na wenzake huko huko Marekani kwa ajili ya mechi za maandalizi.      

Zlatan kurejea Man united kwa sababu hii

Image
Zlatan Ibrahimovic ameonekana katika viwanja vya Manchester bado kuna tetesi kuwa atapewa mkataba wa muda fupi endapo atapona haraka licha ya kutemwa na timu hiyo, mshambuliaji ambaye ametuma video yake mpya inayomuonyesha akifanya mazoezi katika viwanja hivyo vya Manchester united ambapo klabu hiyo imemruhusu kutumia kiwanja na vifaa vyote mpaka atakapopona vizuri au kupata timu nyingine. Ibrahimovic amepona mapema mno tofauti na matarijio ya wengi baada taarifa za mwanzo za matibabu zikionyesha kuwa angekuwa nje kwa muda wa miezi sita huku akihusishwa pia na kutimkia spain ili kujiunga na Atletico madrid au kutimkia Marekani.        

Rooney apishana na Lukaku Manchester united

Image
Klabu ya Manchester united yakubali kutoa paund milioni 75 kwa klabu ya Everton ili kukamilisha usajili wa Romelo Lukaku. Mshambuliaji huyo alifanikiwa kufunga magoli 71 katika michezo 133 aliyocheza tangu ajiunge na klabu hiyo mwaka 2014 . Manchester united imefanikiwa kuziba pengo la Ibrahimovic aliyeachwa huru mwishoni mwa msimu huu kwa kumnasa mshambuliaji huyo mwenye miaka 24 kama mbadala wa muda mrefu huku klabu ya Everton ikipewa nafasi kubwa ya kumrudisha Wayne Rooney msimu huu.    

Rooney aondoka ili kupisha usajili mpya Manchester

Image
Mchezaji wa man utd Wayne Rooney aondolewa katika kikosi cha Manchester united kitakachosafiri siku tano zijazo ili akamilishe usajili wake wa kwenda Everton nakupisha usajili mpya ndani ya klabu ya  Manchester united. Hii inatoa mwanya kwa kiungo wa Real Madrid James Rodriguez kujiunga na klabu ya Manchester United ambapo kikwazo kikubwa ni jezi ya namba 10 inayovaliwa na gwiji huyo wa timu ya Manchester anayeshikiliya record ya kuwa mfungaji wa mda wote katika klabu hiyo. Ambapo mkataba wa adidas unamlazimisha James kuvaa jezi yenye namba 10 katika timu yoyote atakayochezea. James Rodriguez amekuwa akihusihwa na kujiunga na klabu hiyo kabla dirisha kubwa la usajili kufunguliwa na mchezaji huyo amewahi kuzitema ofa nyingi ikiwemo ile ya kutoka klabu ya Inter Milan ili apate kujiunga na klabu ya mashetani wekundu wa jiji la Manchester.
Mchezaji wa man utd Wayne Rooney aondolewa katika kikosi cha Manchester united kitakachosafiri siku tano zijazo ili akamilishe usajili wake wa kwenda Everton nakupisha usajili mpya ndani ya klabu ya  Manchester united. Hii inatoa mwanya kwa kiungo wa Real Madrid James Rodriguez kujiunga na klabu ya Manchester United ambapo kikwazo kikubwa ni jezi ya namba 10 inayovaliwa na gwiji huyo wa timu ya Manchester anayeshikiliya record ya kuwa mfungaji wa mda wote katika klabu hiyo. Ambapo mkataba wa adidas unamlazimisha James kuvaa jezi yenye namba 10 katika timu yoyote atakayochezea. James Rodriguez amekuwa akihusihwa na kujiunga na klabu hiyo kabla dirisha kubwa la usajili kufunguliwa na mchezaji huyo amewahi kuzitema ofa nyingi ikiwemo ile ya kutoka klabu ya Inter Milan ili apate kujiunga na klabu ya mashetani wekundu wa jiji la Manchester.

Man united yasajili mshambuliaji mpya

Image
Mtandao wa Manchester umethibisha kumsaini mshambuliaji Largie Ramadhan katika klabu ya Manchester united na amesaini mkataba wa miaka minne.                                         largie ramazan Mshambuliaji mwenye umri wa miaka 16 anaungana na wachezaji wenzake wawili ambao ni Aliou Badara Traore na Ethan Galbraith wote wakiwa ni akademi waliosajiliwa na klabu hiyo katika dirisha hili kubwa la usajili. Ramazani anatokea katika klabu ya Anderlecht kutoka ubelgiji baada ya kuwavutia sana skauti wa Manchester united kabla ya kumwaga wino.

Baba wa Morata aingilia kati swala la usajili wa mwanae

Image
Mshambuliaji wa Real madrid anayehusishwa vikali na kujiunga na klabu ya Man united Alvaro morata amemtuma wakala wake ambaye ni baba yake mzazi aitwae Alfonso Morata ashinikize haraka usajili wake kuelekea klabu ya Man united. Kwa sasa ipo wazi kuwa Mourinho anasaka saini ya mchezaji huyo wa Madrid ili kuziba pengo la Ibrahimovic alieachwa kama mchezaji huru mwishoni mwa msimu ulioisha.Asubuhi ya leo Alfonso alionekana akitoka katika office ya klabu ya Real madrid kama ilivyoarifiwa na vyombo vya habari vya spain. Kocha wa Manchester United, Jose Mourinho anataka kukamilisha usajili huo mapema kabla ya mechi za maandalizi kwa ajili ya msimu ujao. mimiunited

Mambo 10 usioyajua kumhusu Wayne Rooney

Image
Mshambuliaji wa Man united mwenye mafanikio makubwa ambayo kila mchezaji anaota kuyafikia katika kazi yake hiyo kuanzia klabu yake ya Man united hadi timu ya taifa, haya ni baadhi ya mambo ambayo huyajui kumhusu yeye 1> Akiwa na Everton katika kikosi cha wachezaji wa chini miaka 11 Rooney alifunga magoli 114 katika michezo  30. 2> Steve Rutter wakati akiwa.kocha wa timu ya taifa ya Uingereza chini ya miaka 15 hakutegemea kama Rooney angekuwa kapteni wa Uingereza au moja ya  mshambuliaji bora duniani kutokana na kutoamini uwezo wake kwa kuamini kwake kuwa hakustahili kucheza nafasi ya mshambuliaji badala yake akamuweka winga na sio mshambuliaji. 3> Akiwa na miaka 14 tu Rooney alifanikiwa kupata mkataba wake wa kwanza na UMBRO uliompatia pound elf 2 kwa mwaka. 4> Ana matatizo ya macho tangu akiwa mdogo alipimwa macho na kupewa miwani lakini ni mara Mjue Rooney chache tu ambapo Rooney alivaa hiyo miwani. 5> Rooney alihoji kuhusu mbinu za ufundishaji ...

Magoli yote 11 aliyofunga Mikhtaryan yaone hapa

Image

Alichosema Zlatan baada ya kuachwa na Man united hiki hapa

Image
Aliyekuwa mshambuliaji wa Man united ya uingereza tayari amewaaga mashabiki wa ligi hiyo baada ya kuacha ujumbe unaoashiria kuwa hataendelea  kuchezaa ligi hiyo,ni baada ya kujibu ujumbe wake mwenyewe wa Instagram aliotuma miaka mitatu iliyopita kitu kinachoonyesha ni kama utabiri aliojitabiria mwenyewe,ujumbe huo wa mwanzo wa mwaka 2014 ulisema kuwa "kama ningechezea ligi kuu ya Uingereza nako ningeharibu kama ninavyofanya katika ligi nyingine". Ibrahimovic licha ya kuhamia ligi kuu ya Uingereza huku akiwa na umri wa miaka 35 bado aliweza kufunga magoli 17 katika michezo 28 aliyocheza na kuandika tena ujumbe mwaka 2017 unaosema kuwa "Mimi ni Zlatan Ibrahimovic nimethibitisha nilikuja nikasema napenda kushinda " Ibrahimovic amemkosoa Arsene Wenger aliyeponda usajili wake kwakusema ni usajili wake ni mzuri lakini umechelewa akiimanisha umri ni mkubwa hivyo hautakuwa na matokeo mazuri lakini imekuwa tofaut i kwani Ibrahim...

Morata achoshwa na benchi amwambia rafiki yake wa karibu kuwa anajiunga na Manchester united

Image
Mshambuliaji wa Real Madrid anayehusishwa sana na kuelekea jijini Manchester, Alvaro Morata ili kujiunga na mashetani hao wekundu kila siku zinavyoenda taarifa zinazidi kukua ya kwamba anakaribia kusaini katika klabu ya Man united inayoongozwa na kocha mtukutu Jose Mourinho hii ni baada ya kumwambia rafiki yake wa karibu kuwa anajiunga na Mashetani hao wa jiji la Manchester na kwenda kuungana na nyota wenzake wa spain kama Mata , De gea na herrera . Kocha wa Manchester anahangaika kuipata saini ya mshambuliaji huyo wa Real Madrid ili kuziba pengo la Ibrahimovic mshambuliaji alieipa mafanikio makubwa klabu hiyo msimu uliopita, Morata ni kijana alielelewa katika klabu ya real japo ameshindwa kupata nafasi ya kudumu katika klabu hiyo jambo lililompelekea kujiunga na klabu ya Juventus kwa mkopo kabla ya kurejea tena.      Je Morata ni chaguo sahihi katika kukipa mafanikio kikosi hicho cha Man united ?

Man united iliipotezea nafasi ya kumsajili Saul Niguez

Image
Klabu ya Manchester united ya nchini  Uingereza iliipoteza nafasi ya kumsajili kiungo mkabaji wa Atletico Madrid mwaka 2013 kwa bei ya chini wakati kiungo huyo akitafuta nafasi ya kucheza katika klabu nyingine. Atletico waliwapa nafasi ya kumnunua klabu ya Manchester ambao hata hivyo nao hawakuwa tayari kumchukua wakati ikiwa chini ya kocha David Moyes alienda yeye na baba yake Carrington mwaka huo ambapo hata hivyo dili liliharibika baadae, kiungo huyo ambaye kwa sasa thamani yake inakadiriwa kufika Pound m.71. Saul Niguez kwa sasa anawania vikali na klabu ya Barcelona kwa dau nono. Saul Niguez ambae staili yake ya uchezaji inafananishwa na  kiungo wa barcelona Sergio Busquet kukaba kwa nguvu na kutengeneza mashambulizi ni mchezaji ambae Man united ingemuhitaji sana msimu uliopita .

Wajue wachezaji watano wa Manchester United waliovunja record msimu wa 2016 - 2017

Image
Manchester United imemaliza msimu wake wa kwanza kwa kocha Jose Mourinho huku akifanikiwa kuipa vikombe vitatu na kuwa kocha wa kwanza wa Manchester United kufanya hivyo kwa msimu wa kwanza tu. Na pia kuna baadhi ya wachezaji watano ambao wamejiwekea record zao ndani ya klabu hiyo ambao ni.               POGBA : Ni kiungo wa Manchester United alierejeshwa klabuni akitokea Juventus huku akivunja record ya kuwa mchezaji ghali zaidi wa mpira duniani na pia Pogba kwa anashikilia record ku retweet post zake za tweeter.                                           IBAHMOVIC : Ni mchezaji alievunja record nyingi katika kazi yake ya soka hakuishia hapo kwani aliendelea kuvunja record hata alipofikia umri wake wa miaka 35 pale alipofunga magoli 15 na kuwa mchezaji pekee wa umri wake kufikisha magoli kama hayo akiwa na umri wa miaka 35 ndani ya  ...

Perez akana kuzungumza na man united juu ya morata

Image
Rais wa Real Madrid ambao ndio mabingwa wa la liga na mabingwa wa klabu bingwa barani ulaya amekanusha vikali taarifa za kuwa tayari wamefanya mazungumzo na united juu ya kuwauzia Morata. Taarifa zilizosambaa ni kuwa Morata anakaribia kutua katika klabu ya Manchester united kwa dau nono huku Perez akisema kuwa amesoma hizi habari zaidi mara million lakini hizi taarifa si za kweli. Morata ambae amecheza mechi 14 tu msimu ulioisha huku akishinda magoli 20 katika mashindano yote inaaminika kuwa anaelekea Manchester United kwenda kupata nafasi ya kucheza zaidi