Rooney aaga rasmi na wachezaji wakitoa maneno yao

Safari ya aliekuwa mchezaji wa Manchester united Wayne Rooney imefika na amekamilisha usajili wake na kurudi katika klabu yake ya utotoni ya Everton.
Rooney ameiaga rasmi klabu yake hiyo aliochezea muda mrefu  Manchester ambayo ilimsajili kutoka Everton mwaka 2004 na akaitumikia kwa muda wa miaka 13 huku akishinda vikombe 16 na kuvunja record ya ufungaji katika klabu hiyo.
Ametuma katika mitandao kijamii amesema "Nataka kutoa shukran kubwa kwa kila mtu hapa Manchester"
"Shukran kwa bodi nzima, na makocha niliocheza chini yao, na wafanyakazi wote tuliofanya kazi pamoja, na wachezaji wote tuliocheza pamoja na mwisho ni mashabiki wazuri ambao nimebahatika kucheza chini yao, Ahsanteni."
Baada ya hapo ni wachezaji ambao amecheza nao walionyesha hisia zao kupitia mitandao ya kijamii kama vile
Daley Blind: Kila la heri @WayneRooney and na asante kwa kila kitu. #Gwiji
Tim Fosu-Mensah: Kwaheri gwiji, @WayneRooney. Nahisi kuheshika kwa kuweza kucheza na wew. #Legend
Ander Herrera: Ipo siku nitawaambia wajukuu zangu kuwa nilicheza na wewe. Kila la heri @WayneRooney. #Kwaheri gwiji.

Comments

Popular posts from this blog

Tetesi za usajili Man united

Wajue wachezaji watano wa Manchester United waliovunja record msimu wa 2016 - 2017

Taarifa mpya za klabu ya Manchester United