Takwimu ya wachezaji wa Man United dhidi ya Real Salt

J.Pereira : Ameokoa michomo miwili hatari japo alifungwa lakini ni goli ambalo hata kipa bora duniani angeweza kufungwa. 3.5/5

P.Jones : Alikosa umakini kidogo kiasi cha kuigharimu timu hadi kufungwa. 2.5/5

D.Blind : Hana kasi kubwa katika kupanda na kushambulia huku akirudi nyuma kulinda goli lakini ni mchezaji ambae ana uwezo mkubwa wa kukaba kama alivyofanya leo.2.5/5

V.Lindelof : Amerudi tena leo kwa mara ya pili na kama ilivyo kawaida yake alitulia uwanjani na kutoa pasi nzuri kama linavyosema jina lake la utani mtu wa barafu(iceman). 3.5/5

T.Fosu-Mensah : Alionesha ubora wake kwa kulinda huku akipanda na kushuka alikuwa pia akishirikiana vizuri na wenzake wenzake uwanjani. 3.5/5

S.Mctominay : Ameonyesha kujiamini uwanjani na hakusita kwenda mbele kila alipopata mipira. 3.5/5

M.Carrick : Hakuwa katika ubora wake leo kwa kushindwa kumiliki mipira. 2/5

P.Pogba : Alipoteza mipira mingi uwanjani lakini baadae alibadilika na kucheza vizuri kiasi. 2.5/5

H.Mkhtaryan : Ameshinda goli amecheza vizuri japo alikuwa na mwanzo mbovu. 3/5

J.Lingard : Alikuwa moto siku ya leo ameonyesha ushirikiano mzuri na Lukaku uwanjani pia alikuwa akijipanga vizuri. 3/5

R.Lukaku : Amesaidiana vyema na Lingard ameshinda goli lake la kwanza Man Utd ni goli ambalo limewarudisha mchezoni siku ya leo. 4.5/5

Wachezaji wa akiba

S.Romero : Hakuwa na kazi kubwa golini lakini aliweza kuisaidia timu yake isifungwe kwa kuokoa mchomo mkali na kuifanya timu iibuke kidedea. 2.5/5

C.Smalling : Ilibaki kidogo aipatie timu yake bao baada ya kupokea pasi maridadi kutoka kwa Pereira. 3/5

E.Baily : Alifanya kama alivyotumwa hakuwapa nafasi wapinzani wake hata ya kukaa golini. 3/5

A.Valencia : Alipewa kadi nyekundu mapema tu japo haikuwa halali. 3/5

M.Darmian : Amecheza vizuri sana lakini katika idara yake ya ulinzi ila ni mzito sana katika kupandisha timu.

A.Herrera : Amecheza vizuri mwanzoni lakini pia alipoza sana mpira kumiliki sana. 2.5/5

A.Pereira : Alikuwa mzuri sana katika mchezo kwa kutoa pasi fupi fupi zenye faida kwa timu. 3.5/5

M.Fellaini : Amekuwa na mchezo mbaya pasi mbovu zinazoishia njiani bila ya kumfikia mlengwa. 2/5

D.Mitchell : Ameonyesha kiwango kizuri kiasi cha kumshawishi kocha amuangalie msimu ujao. 4/5

A.Martial : Aliwakimbiza sana mabeki kiasi cha kuwatia hofu wasitoke golini mwao lakini hakuwa maamuzi ya mwisho. 3.5/5

M.Rashford : Ameendelea kung'ara uwanjani kwa kuwasumbua mabeki wa Real Salt lakini alikosa mtu kumtupia krosi. 3.5/5

J.Mata : Hakupata nafasi ya kucheza dakika za mwisho.

A.Tuanzebe : Hakupata nafasi

Comments

Popular posts from this blog

Tetesi za usajili Man united

Wajue wachezaji watano wa Manchester United waliovunja record msimu wa 2016 - 2017

Taarifa mpya za klabu ya Manchester United