Wajue wachezaji watano wa Manchester United waliovunja record msimu wa 2016 - 2017

Manchester United imemaliza msimu wake wa kwanza kwa kocha Jose Mourinho huku akifanikiwa kuipa vikombe vitatu na kuwa kocha wa kwanza wa Manchester United kufanya hivyo kwa msimu wa kwanza tu.
Na pia kuna baadhi ya wachezaji watano ambao wamejiwekea record zao ndani ya klabu hiyo ambao ni.
           

  POGBA : Ni kiungo wa Manchester United alierejeshwa klabuni akitokea Juventus huku akivunja record ya kuwa mchezaji ghali zaidi wa mpira duniani na pia Pogba kwa anashikilia record ku retweet post zake za tweeter.
                                       

  IBAHMOVIC : Ni mchezaji alievunja record nyingi katika kazi yake ya soka hakuishia hapo kwani aliendelea kuvunja record hata alipofikia umri wake wa miaka 35 pale alipofunga magoli 15 na kuwa mchezaji pekee wa umri wake kufikisha magoli kama hayo akiwa na umri wa miaka 35 ndani ya  ligi kuu ya uingereza msimu uliopita wa 2016 - 2017.
                                       
ROONEY : Rooney atabaki kukumbukwa na mashabiki wa Manchester kwa magoli yake muhimu aliowahi kuwafungia Man United likiwemo lile goli lake la tiktak dhidi ya watani wao wa jadi Man city, Rooney msimu uliopita alifunga tena goli muhimu likitokana na mpira wa adhabu dhidi ya Stoke city akibadili matokeo na kuwa 1 - 1 huku akiweka record kwa kufikisha magoli 250 na kuvunja record ya muda mrefu iliyowekwa na Sir Bobby Charlton ya magoli 249.
                      
                                      
MIKHITARYAN : Unaweza pia kumuita Micki Magic ni mchezaji wa Man united mwenye kipaji cha hali ya juu ukiwa ni msimu wake wa kwanza tu tangu ajiunge na Man United akitokea Dortmund ya Ujeruman tayari amejipatia umaarufu mkubwa na kujiwekea record ndani ya klabu hiyo kwa  kushinda goli la pili katika mechi ya fainal dhidi ya Ajax na kuwa mchezaji wa kwanza wa klabu hiyo kufunga magoli matano katika michezo tofauti ya kombe la Europa huku mengine akifunga dhidi ya Zorya Luhansk, Saint-Etienne, Rostov na Anderlecht.
 
                                         

 A.GOMES : Katika mchezo wa mwisho wa mwisho wa wa Premier league dhidi ya Crystal Palace ilikuwa ni siku nzuri kwa Josh Harrop lakini haikuishia hapo kwani ilikuwa pia ni mechi ya kwanza ya Angel Gomes ambae aliweka record mpya ya kuwa mchezaji mwenye umri mdogo zaidi ndani ya klabu ya Manchester United kucheza na pia ni mchezaji mdogo zaidi wa Premier league tangu afanye hivyo Duncan Edwards ambaye pia alikuwa ni mchezaji wa Manchester.

Comments

Popular posts from this blog

Tetesi za usajili Man united

Taarifa mpya za klabu ya Manchester United