Taarifa mpya za klabu ya Manchester United
Antoine Griezman
Wakala wa zamani wa Griezman amefichua kuwa ilibakia kidogo kwa mchezaji kujiunga na klabu ya Man united baada ya klabu yake anayoichezea ya Atletico Madrid kufungiwa kutokusajili.
Taarifa zikisema kuwa klabu zote mbili zilikubaliana usajili wa mchezaji huyo kwa dau la euro milioni 100.
Ivan Perisic
Mchezaji anaewindwa vikali na klabu ya Manchester United Perisic, 28, anategemea kuongeza mkataba na klabu yake ya Inter Milan baada ya timu hiyo ya jiji la Milan kugoma kuwauzia mabingwa wa kombe la FA na Europa Man United.
Milan watamuongezea mkataba hivi karibuni ili kuwakatisha tamaa Mashetani juu ya kumsajili winga huyo machachari.
Luke Shaw
Beki wa kushoto raia wa Uingereza Luke Shaw anatarajia kuongezewa mkataba wa kuendelea kukipiga katika klabu ya Manchester United licha ya kuwa na majeruhi ya mara kwa mara bado kocha wa timu hiyo ameonyesha kuwa na matumaini na mchezaji huyo.
Serge Aurier
Beki wa PSG , Aurier ameichagua Manchester United badala ya Tottenham iliopeleka dau la Paund milion 23 na kukubaliwa na PSG lakini inaarifiwa kuwa mchezaji huyo haitaki klabu hiyo badala yake amechagua kujiunga na Mashetani wekundu wa jiji la Manchester.

Comments
Post a Comment