Mkhtaryan na record mpya dhidi ya Leicester

Mkhtaryan aweka record baada ya mchezo wake dhidi ya Leicester kwa kutoa assist kwa mchezaji Rashford na kuwa mchezaji pekee kufanya hivyo kwa kutoa assist tano katika michezo mitatu ya mwanzo ambapo imekuwa ni haraka zaidi kwa mchezaji wa ligi kuu ya Uingereza kuwahi kufanya hivyo akiwa sambasamba na Ruel Fox wa Newcastle aliyefikisha pasi kama hizo za magoli tano katika michezo mitatu ya mwanzo tokea msimu wa 1994/95.
Mkhtaryan alitoa pasi mbili katika mchezo wao wa kwanza dhidi ya West ham kwa kutoa assist kwa wachezaji Lukaku na Martial na kuendeleza kazi yake hiyo katika mchezo uliofuata dhidi ya Swansea akitoa tena pasi mbili kwa wachezaji Lukaku na Pogba na akimaliza kazi yake kwa Leicester mara hii akitoa assist kwa Rashford huku Klabu ya Manchester ikifikisha magoli 10 katika michezo mitatu.

Comments

Popular posts from this blog

Tetesi za usajili Man united

Wajue wachezaji watano wa Manchester United waliovunja record msimu wa 2016 - 2017

Taarifa mpya za klabu ya Manchester United