Evra atoa povu lake mtandaoni
Mchezaji wa zamani Manchester ambae haishiwi na vituko mitandaoni Patrice Evra ameibuka tena mpya baada ya kuwaponda wanaomzarau akiwemo na mwalimu wake mwalimu wake aliemwambia kuwa huwezi soka kwa sababu wewe ni mfupi.
Evra amezoweleka kwa kutumia video mbalimbali mtandaoni akisema maneno kama "I love this game" akimaanisha kuwa huu mchezo naupenda mara hii amekuwa tofauti baada ya kutuma video inayomuonyesha akiwa mazoezini huku akisema "usiwe na wivu japo walisema siwezi sasa nina vikombe zaidi ya 21 nimecheza fainali nyingi na nimeshinda japo nimepoteza nyingi lakini nimeshinda makombe mengi na bado nahitaji makombe mengi zaidi" na akimaliza kuwa "I love this game"
Comments
Post a Comment