Tetesi za usajili Man united

Tottenham na Inter Milan kwa pamoja zimeingia katika mbio ya kumuwania beki wa PSG na anaewindwa na Manchester united Sergi Aurier beki huyo wa PSG na Raia wa Ivory coast anahusishwa vikali na kujiunga na Man utd.
Chanzo : La Parisien


Klabu ya Manchester united inamfatilia kiungo wa Anderlecht aitwae Leander Dendocker.
Mashetani hao wekundu wametuma scout ili kumfatilia kiungo ambae alifunga goli walipokutana na timu hiyo katika mashindano ya Europa League, mchezaji huyo kwa sasa ana miaka 22, Kocha wa united anamtaka kiungo huyo kwa msimu ujao.
Lakini pia mchezaji huyo anawindwa na klabu za Leipzig na Ac Milan ya Italia.
Chanzo : The Mirror
               
Klabu ya Watford inataka kumsajili kinda wa Man utd Timothy Fosu-Mensah kwa mkopo kinda wa United mwenye uwezo wa kucheza kama beki wa pembeni,kiungo mkabaji na beki wa kati hatma yake kuamuliwa baada ya mchezo wa dhidi ya Real Madrid.
Chanzo : Dail Mail
             
Juan Mata anafanya maongezi na klabu yake ya Man utd ili kuongeza mkataba wake.Kiungo huyo Mhispania anategemewa kuongeza mkataba yeye na kiungo mwenzake raia wa spain Ander Herrera hivi karibuni.
Chanzo : ESPN
                   

Comments

Popular posts from this blog

Wajue wachezaji watano wa Manchester United waliovunja record msimu wa 2016 - 2017

Taarifa mpya za klabu ya Manchester United