Man united kusajili watatu wiki hii

Mtendaji mkuu wa klabu ya Manchester united Ed  Woodward amebaki jijini ili kuhakisha kuwa anakamilisha biashara ya kuwasajili wachezaji watatu ndani ya wiki hii taarifa kutoka mtandao wa Manchester Evening News imesewa kuwa Woodward alitakiwa kuhudhuria mjini Houston ili kushuhudhia mchezo wa Manchester derby lakini ameshindwa kutokana na majukumu yake ya kazi ili kuhakikisha kuwa anafanikisha dili la wachezaji Dier,Perisic na Matic  au wawili kati yao na ikishindikana wawili basi hata mmoja wao mapema wiki hii.
Kocha huyo mbwatukaji wa Manchester united kwa sasa bado hajaonana na mtendaji huyo tangu aseme waziwazi kuwa hafurahishwi na utendaji wa kazi wa klabu yake katika idara ya hiyo kwa kushindwa kuwasajili mapema orodha ya majina ya wachezaji alioiwasilisha.

Comments

Popular posts from this blog

Tetesi za usajili Man united

Wajue wachezaji watano wa Manchester United waliovunja record msimu wa 2016 - 2017

Taarifa mpya za klabu ya Manchester United