Renato Sanchez anukia Manchester United
Baada ya kocha wa Bayern Munich kusema kuwa mchezaji wa timu hiyo Renato Sanchez anaweza kutimkia timu nyingine katika dirisha hili kubwa la usajili mara hii ni mchezaji mwenyewe Sanchez ambae amethibisha kuwa anaondoka msimu huu na kutimkia timu nyingine ili kupata nafasi ya kucheza mara kwa mara, Sanchez amesema maneno hayo baada ya kumalizika kwa mchezo wao dhidi ya Chelsea na kuichabanga kwa magoli 3 kwa 2.
Bayern hawapo tayari kumuuza mchezaji badala yake wanategemea kumpeleka kwa mkopo kwa mashetani wa jiji la Manchester huo utakuwa ni usajili wa tatu kufanywa na klabu hiyo ambayo pia inawawania wachezaji kama Marco Verrati na Perisic.
Sanchez aliwahi kuikacha Manchester united na kabla ya kusaini Bayern lakini kikwazo ni kuwa pia kinda huyo anawindwa pia na klabu ya AC Milan ya Italia ambapo akiizungumzia Milan amesema yupo tayari kujiunga nao endapo watatoa ofa sahihi kwa klabu yake na kukubaliana pande zote mbili kwa kusema AC Milan atapata nafasi zaidi ya kucheza kuliko Bayern Munich ya Ujerumani.

Comments
Post a Comment