Zlatan kurejea Man united kwa sababu hii
Zlatan Ibrahimovic ameonekana katika viwanja vya Manchester bado kuna tetesi kuwa atapewa mkataba wa muda fupi endapo atapona haraka licha ya kutemwa na timu hiyo, mshambuliaji ambaye ametuma video yake mpya inayomuonyesha akifanya mazoezi katika viwanja hivyo vya Manchester united ambapo klabu hiyo imemruhusu kutumia kiwanja na vifaa vyote mpaka atakapopona vizuri au kupata timu nyingine.
Ibrahimovic amepona mapema mno tofauti na matarijio ya wengi baada taarifa za mwanzo za matibabu zikionyesha kuwa angekuwa nje kwa muda wa miezi sita huku akihusishwa pia na kutimkia spain ili kujiunga na Atletico madrid au kutimkia Marekani.
Comments
Post a Comment