Baba wa Morata aingilia kati swala la usajili wa mwanae

Mshambuliaji wa Real madrid anayehusishwa vikali na kujiunga na klabu ya Man united Alvaro morata amemtuma wakala wake ambaye ni baba yake mzazi aitwae Alfonso Morata ashinikize haraka usajili wake kuelekea klabu ya Man united.
Kwa sasa ipo wazi kuwa Mourinho anasaka saini ya mchezaji huyo wa Madrid ili kuziba pengo la Ibrahimovic alieachwa kama mchezaji huru mwishoni mwa msimu ulioisha.Asubuhi ya leo Alfonso alionekana akitoka katika office ya klabu ya Real madrid kama ilivyoarifiwa na vyombo vya habari vya spain.
Kocha wa Manchester United, Jose Mourinho anataka kukamilisha usajili huo mapema kabla ya mechi za maandalizi kwa ajili ya msimu ujao.
mimiunited

Comments

Popular posts from this blog

Tetesi za usajili Man united

Wajue wachezaji watano wa Manchester United waliovunja record msimu wa 2016 - 2017

Taarifa mpya za klabu ya Manchester United