Viwango vya wachezaji wa Man United na video highlight ya mchezo dhidi ya Man city

Kocha Jose Mourinho amepambana tena na Guardiola na kuibuka na ushindi wa goli mbili kwa bila na mchezaji Lukaku akiendelea kung'ara tena na kufunga goli moja katika mchezo huo.
Hivi ni viwango vya wachezaji wa man united katika mchezo wa leo.

De Gea : Ameokoa michomo miwili hatari kuifanya Man united iendelee kuongoza. 4/5

A.Valencia : Alipanda na kushuka golini kwa kasi kuisaidia timu vizuri mchezaji alieanza kama kapteni wa timu kabla ya kumpa Carrick kipindi cha pili. 4/5

V.Lindelof : Alifanya kosa moja kiasi liigharimu timu, Alikuwa ni mwiba mkali kwa Aguero kwa kumkaba vilivyo. 3.5/5

D.Blind : Hakuwa fomu siku ya leo, na kuhenyeshwa vilivyo na Patrick Roberts kwa mtazamo ni vyema akicheza kati. 3/5

C.Smalling : Kuna wakati alicheza vizuri lakini kuna wakati aliharibu na ilikuwa ni bahati kwake kutowapa city penati. 3/5

P.Pogba : Ana uwezo mkubwa wa kutoa pasi aliwasumbua sana wachezaji wa Manchester city na vitu vyake vingi na adimu kuviona kwa mchezaji. 4/5

H.Mkhtaryan : Huku akicheza katika nafasi yake aliyong'ara Dortmund nyuma ya mshambuliaji namba 10 alionyesha uwezo mkubwa wa kumiliki na kutoa pasi hatari golini mwa City. 4.5/5

A.Herrera : Baada ya kumueka mfukoni Aguero mara hii Mourinho kazi ya kuenda na Toure bila ya makosa alifanya kazi yake hiyo kuhakikisha Yaya Toure nae hafurukuti uwanjani. 4/5

J.Lingard : Mchezaji mwingine aliecheza vyema japo alikuwa na kusua kusua kwa kuzunguka na mipira hadi nje ya uwanja. 3/5

R.Lukaku : Alikimbia vyema uwanjani kila alipokuwa na mpira na kushinda goli maridadi. 4.5/5

M.Rashford : Alikabwa kila pembe na na Paul Walker lakini hilo halikumzuia kupata goli la pili kwa Man united na kuifanya iibuke kidedea siku ya leo. 4/5

Wachezaji wa akiba

S.Romero : Ni kipa mzuri na aliendelea kuonyesha umuhimu kwa kuokoa baadhi ya michomo hatari golini. 3.5/5.

P.Jones : Alimkaba Jesus vyema kuhakikisha haleti usumbufu golini alilinda vizuri na alikuwa mgumu kumpita. 3.5/5

E.Baily : Ni vigumu kumkuta yupo chini ya kiwango akiwa kati kwa kushirikiana vyema mara hii akiwa Jones waliweka ukuta sahihi. 3.5/5

M.Darmian : Amecheza vizuri sitegemei kama Mou atamuachia hata kama alikuwa ana nia ya kumuuza. 3.5/5

A.Pereira : Alikuwa mzuri sana katika mchezo kwa kutoa pasi fupi fupi zenye faida kwa timu. 3/5

M.Fellaini : Amewauzia viungo wa Man City wasipate nafasi ya kuuchezea mpira na kuziba nafasi. 3.5/5

T.Fosu-Mensah : Amekuwa na mwendelezo mzuri kiuchezaji kiujumla nategemea atacheza mechi mingi zaidi msimu unaokuja. 3.5/5

A.Martial : Hakupata nafasi vyema ya kuonyesha uwezo wake uwanjani japo hakuchelewa sana kuingia uwanjanh. 3/5

A.Pereira : Alitulia na kuwasumbua mabeki wa timu pinzani kila alipokuwa na mpira huku akionyesha kujiamini uwanjani. 3.5/5
   
       ushahidi wa video

Comments

Popular posts from this blog

Tetesi za usajili Man united

Wajue wachezaji watano wa Manchester United waliovunja record msimu wa 2016 - 2017

Taarifa mpya za klabu ya Manchester United