Pogba ampongeza Lukaku

Kiungo wa Manchester united, Paul Pogba amemkaribisha Romelu Lukaku katika account yake ya Instagram.
Paul Pogba ametuma video yake akimpongeza mshambuliaji huyo kwa kukamilisha wake uhamisho wake na kuungana na rafiki yake huyo wa muda mrefu.
               https://www.instagram.com/p/BWRuiuthRnJ/?r=wa1
Katika video ambayo Pogba ameandika "tutaonana kesho mazoezini" baada ya klabu ya Manchester united kuthibisha kumsajili aliekuwa mshambuliaji wa Everton Lukaku.
Lukaku akiongea kifaransa anasema "haikuwa kazi rahisi, lakini sasa tumekamilisha, tutaonana kesho. Pogba anamuuliza "umesemaje" Lukaku anamjibu "tutaonana kesho, Unaamini au? Pogba kwa sauti anajibu "ndio mzee".
Lukaku na Pogba wote kwa pamoja wapo Los Angeles ambako lukaku anarajia kufanyiwa vipimo vya afya na kujiunga na wenzake huko huko Marekani kwa ajili ya mechi za maandalizi.
     

Comments

Popular posts from this blog

Tetesi za usajili Man united

Wajue wachezaji watano wa Manchester United waliovunja record msimu wa 2016 - 2017

Taarifa mpya za klabu ya Manchester United