Wenger nusu awe kocha Manchester united

Arsene Wenger alipata nafasi ya kuifundisha Manchester United baada ya Fergie kubwaga manyanga lakini hata hivyo aliikataa kutokana na utiifu wake kwa mwenyekiti wa Arsenal, David Dein amefichua Mwenyekiti wa zamani wa Manchester United Martin Edwards kuwa Wenger alikuwa ni chaguo letu la kwanza baada ya Ferguson kutangaza kustaafu msimu wa  mwaka 2000/01 kabla ya Fergie kubadili maamuzi na kuendelea kufundisha kwa zaidi ya miaka 10 yenye mafanikio makubwa.
Martin asema kuwa "Tulimfata Wenger na alionyesha kuvutiwa na ofa yetu kiasi cha kutukutanisha mimi na Peter Kenyon katika nyumba yake London ili kusikiliza ni vipi tungezungumza."

Edwards anaendelea kuwa kilichomfanya Wenger abaki ni utii wake kwa uongozi wa Arsenal kwa sababu Wenger alikuwa karibu sana na David Dein kitu kilichomfanya ashindwe kuondoka bila ya ridhaa ya uongozi wake.

Comments

Popular posts from this blog

Tetesi za usajili Man united

Wajue wachezaji watano wa Manchester United waliovunja record msimu wa 2016 - 2017

Taarifa mpya za klabu ya Manchester United