Mourinho amsifu Pareira kwa kuongeza mkataba mpya

Pareira ameongeza mkataba wake wa kukipiga OT licha ya kusajiliwa na Valencia ya Spain kwa mkopo mwishoni mwa dirisha kubwa la usajili.
Mkataba huo mwaka ambao utamuweka klabuni hapo hadi msimu wa mwaka 2018- 19.
   
        Mou amemuelezea kijana huyo kama atakuwa mchezaji mkubwa na tegemeo hapo baadae mreno huyo amesema.
  "Pareira ni mchezaji mzuri tayari ni mchezaji mdogo mwenye uwezo wa hali ya juu na mwenendo mzuri katika kuendeleza kipaji chake"

  "Sina mashaka kuwa atakuwa mmoja ya wachezaji wakubwa wa hii klabu"
 
  Pareira baada ya kujiunga na Valencia alisema
  "kocha anatengeneza timu nzuri hapa na mimi nataka niwe sehemu ya hiyo timu hivi karibuni"

   "Nitaendeleza uwezo wangu hapa Valencia na natumaini nitapata muda mwingi wa kucheza"

 Pareira amecheza mechi 13 katika timu wa kubwa na kufanikiwa kufunga goli moja mechi yake ya kwanza ilikuwa dhidi ya Tottenham march 2015.

Comments

Popular posts from this blog

Tetesi za usajili Man united

Wajue wachezaji watano wa Manchester United waliovunja record msimu wa 2016 - 2017

Taarifa mpya za klabu ya Manchester United