Man united kumuiba Alexis Sanchez

Manchester united wanafanya mawasiliano ya chini kwa chini na wakala wa Sanchez ili kufanikisha usajili wa kushtukiza kwa kuwapora wapinzani wao wakubwa katika jiji la Manchester klabu ya Manchester City ambao tayari wameshafanya mazungumzo nae. Alexis amekuwa njia panda katika dirisha hili la usajili baada ya kugoma kuongeza mkataba mpya katika klabu yake ya sasa ya Arsenal ili atue klabu mpya yenye kiu ya mataji na itayoshiriki klabu bingwa. Mourinho ni mshabiki mkubwa wa mchezaji huyo raia wa Chile lakini ni kazi ngumu kumsajili mchezaji kutokana na uwepo wa kocha Guardiola katika klabu ya Manchester city aliewahi kufanya kazi na mchezaji huyo katika klabu ya Barca. Sanchez ataelekea Man united kama mbadala wa Perisic baada ya kushindwa kumsajili kutoka Milan ya Italy inayokaribia kumuongezea mkataba hivi karibuni.