Posts

Showing posts from June, 2017

Alichosema Zlatan baada ya kuachwa na Man united hiki hapa

Image
Aliyekuwa mshambuliaji wa Man united ya uingereza tayari amewaaga mashabiki wa ligi hiyo baada ya kuacha ujumbe unaoashiria kuwa hataendelea  kuchezaa ligi hiyo,ni baada ya kujibu ujumbe wake mwenyewe wa Instagram aliotuma miaka mitatu iliyopita kitu kinachoonyesha ni kama utabiri aliojitabiria mwenyewe,ujumbe huo wa mwanzo wa mwaka 2014 ulisema kuwa "kama ningechezea ligi kuu ya Uingereza nako ningeharibu kama ninavyofanya katika ligi nyingine". Ibrahimovic licha ya kuhamia ligi kuu ya Uingereza huku akiwa na umri wa miaka 35 bado aliweza kufunga magoli 17 katika michezo 28 aliyocheza na kuandika tena ujumbe mwaka 2017 unaosema kuwa "Mimi ni Zlatan Ibrahimovic nimethibitisha nilikuja nikasema napenda kushinda " Ibrahimovic amemkosoa Arsene Wenger aliyeponda usajili wake kwakusema ni usajili wake ni mzuri lakini umechelewa akiimanisha umri ni mkubwa hivyo hautakuwa na matokeo mazuri lakini imekuwa tofaut i kwani Ibrahim...

Morata achoshwa na benchi amwambia rafiki yake wa karibu kuwa anajiunga na Manchester united

Image
Mshambuliaji wa Real Madrid anayehusishwa sana na kuelekea jijini Manchester, Alvaro Morata ili kujiunga na mashetani hao wekundu kila siku zinavyoenda taarifa zinazidi kukua ya kwamba anakaribia kusaini katika klabu ya Man united inayoongozwa na kocha mtukutu Jose Mourinho hii ni baada ya kumwambia rafiki yake wa karibu kuwa anajiunga na Mashetani hao wa jiji la Manchester na kwenda kuungana na nyota wenzake wa spain kama Mata , De gea na herrera . Kocha wa Manchester anahangaika kuipata saini ya mshambuliaji huyo wa Real Madrid ili kuziba pengo la Ibrahimovic mshambuliaji alieipa mafanikio makubwa klabu hiyo msimu uliopita, Morata ni kijana alielelewa katika klabu ya real japo ameshindwa kupata nafasi ya kudumu katika klabu hiyo jambo lililompelekea kujiunga na klabu ya Juventus kwa mkopo kabla ya kurejea tena.      Je Morata ni chaguo sahihi katika kukipa mafanikio kikosi hicho cha Man united ?

Man united iliipotezea nafasi ya kumsajili Saul Niguez

Image
Klabu ya Manchester united ya nchini  Uingereza iliipoteza nafasi ya kumsajili kiungo mkabaji wa Atletico Madrid mwaka 2013 kwa bei ya chini wakati kiungo huyo akitafuta nafasi ya kucheza katika klabu nyingine. Atletico waliwapa nafasi ya kumnunua klabu ya Manchester ambao hata hivyo nao hawakuwa tayari kumchukua wakati ikiwa chini ya kocha David Moyes alienda yeye na baba yake Carrington mwaka huo ambapo hata hivyo dili liliharibika baadae, kiungo huyo ambaye kwa sasa thamani yake inakadiriwa kufika Pound m.71. Saul Niguez kwa sasa anawania vikali na klabu ya Barcelona kwa dau nono. Saul Niguez ambae staili yake ya uchezaji inafananishwa na  kiungo wa barcelona Sergio Busquet kukaba kwa nguvu na kutengeneza mashambulizi ni mchezaji ambae Man united ingemuhitaji sana msimu uliopita .

Wajue wachezaji watano wa Manchester United waliovunja record msimu wa 2016 - 2017

Image
Manchester United imemaliza msimu wake wa kwanza kwa kocha Jose Mourinho huku akifanikiwa kuipa vikombe vitatu na kuwa kocha wa kwanza wa Manchester United kufanya hivyo kwa msimu wa kwanza tu. Na pia kuna baadhi ya wachezaji watano ambao wamejiwekea record zao ndani ya klabu hiyo ambao ni.               POGBA : Ni kiungo wa Manchester United alierejeshwa klabuni akitokea Juventus huku akivunja record ya kuwa mchezaji ghali zaidi wa mpira duniani na pia Pogba kwa anashikilia record ku retweet post zake za tweeter.                                           IBAHMOVIC : Ni mchezaji alievunja record nyingi katika kazi yake ya soka hakuishia hapo kwani aliendelea kuvunja record hata alipofikia umri wake wa miaka 35 pale alipofunga magoli 15 na kuwa mchezaji pekee wa umri wake kufikisha magoli kama hayo akiwa na umri wa miaka 35 ndani ya  ...

Perez akana kuzungumza na man united juu ya morata

Image
Rais wa Real Madrid ambao ndio mabingwa wa la liga na mabingwa wa klabu bingwa barani ulaya amekanusha vikali taarifa za kuwa tayari wamefanya mazungumzo na united juu ya kuwauzia Morata. Taarifa zilizosambaa ni kuwa Morata anakaribia kutua katika klabu ya Manchester united kwa dau nono huku Perez akisema kuwa amesoma hizi habari zaidi mara million lakini hizi taarifa si za kweli. Morata ambae amecheza mechi 14 tu msimu ulioisha huku akishinda magoli 20 katika mashindano yote inaaminika kuwa anaelekea Manchester United kwenda kupata nafasi ya kucheza zaidi