Posts

Showing posts from September, 2017

Video: Combination ya Matic na Pogba

Image
Wachezaji Matic na Pogba wameonyesha ushirikiano mzuri msimu huu katika sehemu ya kiungo na kuing'arisha timu yao licha ya kutoka sare katika mchezo wao wa mwisho dhidi ya Stoke huku United wakishindwa kuivunja record ya kutoweza kuwafunga Stoke katika uwanja wao wa nyumbani tangu mwaka 2013 yani alipostaf kocha Ferguson katika klabu hiyo. Wachezaji hao wameonyesha kuelewana mapema kama vile walicheza pamoja kwa miaka mitano iliyopita kiasi cha kuwafanya wapinzani wao kuwa na wakati mgumu kwa muda wote kama inavyoonyesha video hii hapa

Jinsi Lukaku alivyoibadilisha Man united mapema tu msimu huu

Image
Kinachoonekana Man United msimu huu ni tofauti na msimu uliopita licha ya mabadiliko madogo tu alioyafanya Mourinho kwa kuwasajili wachezaji ambao hata hivyo mmoja kati yao ameshindwa kupata nafasi kikosini hadi sasa licha ya kuwa wamecheza michezo mitatu ambaye ni Lindelof.  Jina la Lukaku si geni machoni na masikioni mwa watu hususani wapenzi wa ligi kuu ya Uingereza alichokikosa mchezaji ni ladha na utamu wa Champions League (kombe la vilabu vya ulaya) lakini hata hivyo alichokifanya Uingereza huwezi kuwa na mashaka nae juu ya mashindano haya makubwa barani Ulaya na duniani kote mchezo huyo amefanikiwa kufunga magoli matatu katika mechi tatu za mwanzo za ligi na ni manne tukijumuisha mashindano yote yani likiwemo na lile alofunga dhidi ya Madrid.    Lukaku ameifanya Manchester United iwe tishio zaidi mbele tofauti na ilivyokuwa msimu uliopita ikiongozwa na Ibrahimovic wachezaji hawa wote ni wafungaji wazuri lakini Lukaku ni mzuri zaidi licha ya kufanikiwa kufunga mag...

Man united yafanya hatari katika tuzo za ligi kuu Uingereza

Image
Lukaku ametajwa katika majina wachezaji watatu waliochaguliwa kugombea mchezaji bora wa mwezi wa nane(August) huku Manchester ikifanikiwa kutoa majina manne likiwemo la kocha Jose Mourinho anaegombea tuzo ya kocha bora wa mwezi huku mengine yaliotajwa ni Phil jones na Mkhitaryan. Lukaku aliekuwa mchezaji wa Everton amefanikiwa kufunga magoli matatu hadi sasa katika mechi tatu alizocheza ukiacha majina hao wengine wanaogombea ni Morata wa Chelsea, Saido Mane na Salah wote wakiwa wachezaji wa Liverpool na kipa wa Huddersfield aitwae Jonas Lossl.

Mourinho amsifu Pareira kwa kuongeza mkataba mpya

Image
Pareira ameongeza mkataba wake wa kukipiga OT licha ya kusajiliwa na Valencia ya Spain kwa mkopo mwishoni mwa dirisha kubwa la usajili. Mkataba huo mwaka ambao utamuweka klabuni hapo hadi msimu wa mwaka 2018- 19.             Mou amemuelezea kijana huyo kama atakuwa mchezaji mkubwa na tegemeo hapo baadae mreno huyo amesema.   "Pareira ni mchezaji mzuri tayari ni mchezaji mdogo mwenye uwezo wa hali ya juu na mwenendo mzuri katika kuendeleza kipaji chake"   "Sina mashaka kuwa atakuwa mmoja ya wachezaji wakubwa wa hii klabu"     Pareira baada ya kujiunga na Valencia alisema   "kocha anatengeneza timu nzuri hapa na mimi nataka niwe sehemu ya hiyo timu hivi karibuni"    "Nitaendeleza uwezo wangu hapa Valencia na natumaini nitapata muda mwingi wa kucheza"  Pareira amecheza mechi 13 katika timu wa kubwa na kufanikiwa kufunga goli moja mechi yake ya kwanza ilikuwa dhidi ya Tottenham march 2015.

Wenger nusu awe kocha Manchester united

Image
Arsene Wenger alipata nafasi ya kuifundisha Manchester United baada ya Fergie kubwaga manyanga lakini hata hivyo aliikataa kutokana na utiifu wake kwa mwenyekiti wa Arsenal, David Dein amefichua Mwenyekiti wa zamani wa Manchester United Martin Edwards kuwa Wenger alikuwa ni chaguo letu la kwanza baada ya Ferguson kutangaza kustaafu msimu wa  mwaka 2000/01 kabla ya Fergie kubadili maamuzi na kuendelea kufundisha kwa zaidi ya miaka 10 yenye mafanikio makubwa. Martin asema kuwa "Tulimfata Wenger na alionyesha kuvutiwa na ofa yetu kiasi cha kutukutanisha mimi na Peter Kenyon katika nyumba yake London ili kusikiliza ni vipi tungezungumza." Edwards anaendelea kuwa kilichomfanya Wenger abaki ni utii wake kwa uongozi wa Arsenal kwa sababu Wenger alikuwa karibu sana na David Dein kitu kilichomfanya ashindwe kuondoka bila ya ridhaa ya uongozi wake.

Lindelof kuanzishwa mechi hii

Victor Lindelof ni moja ya majina mapya ambayo Mourinho ameyasajili msimu huu lakini mchezaji huyo ameshindwa kupata nafasi ya kucheza tangu ligi ianze huku Manchester wakiwa tayari wameshacheza michezo mitatu ndani ya ligi kuu ya mchezo, hata hivyo Lindelof sio mchezaji pekee aliyekosa nafasi ya kucheza kwani kuna kubwa jingine kama vile beki mwingine wa kati anayetambulika kwa jina la Smalling wote wawili wanatarajia kuanza katika mchezo wa klabu bingwa dhidi ya Basel kwa mujibu wa kocha wa klabu hiyo Jose Mourinho ameweka wazi kuwa atawaanzisha wachezaji wote wawili katika mechi hiyo ya klabu bingwa. Mourinho amesema atakuwa amesema kuwa Lindelof in mchezaji mzuri lakini hana uzoefu na ligi kuu ya Uingereza hivyo anahitaji muda wa kuzoea na kuingia katika mechi zijazo. Lindelof si mchezaji wa kwanza kufanyiwa kama hivyo na Mourinho wapo wengine waliosubirishwa ili waongeze viwango vyao kama vile Wilian akiwa na Chelsea Mikhtaryan na Martial akiwa Manchester.